Maduka ya jumla ya ambayo humilikiwa  na Khetias imefungua tawi la pili la mjini Kakamega huku mkurungunzi mkuu wa maduka hayo na anayesimamia kitengo cha mauzo ya Khetias Ashok Khetia akipongeza kaunti ya Kakamega chini ya gavana Wycliffe Oparanya kwa kuendelea kuwaunga mkono kwa biashara yao jambo anasema limechangia pakubwa kuinua uchumi wa eneo hilo.

Akiongea muda mfupi tu baada ya kufungua duka hilo mpya lililoko mkabala na bustani la Muliro mkurungenzi huyo amesema ufunguzi wa duka hilo umechangia wengi kuajiriwa ambapo zaidi ya watu 70 wamepata ajira kwenye duka hilo.

Kando na kubuni nafasi za ajira kwa wakaazi wa kaunti hiyo, mkurugenzi huyo amesema kuwa wataendelea kutoa usaidizi kwa jamii kwa kuinua masomo kwa wanafunzi ambao hutoka kwa jamii ambazo zinachangamoto za kimapato

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE