Viongozi wa makanisa katika wadi ya Butsotso Mashariki wanaitaka serikali kubuni mbinu ya kutatua ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana kumaliza swala la utumizi wa dawa za kulevya ambazo zimeathiri maisha ya vijana wengi
Wakihutubu kwenye mazishi ya kijana Oliver Munanga eneo la Emusala wakiongozwa na mchungaji Vincent Shikombe wamesema inasikitisha vijana wengi kushindwa kumudu elimu na kukosa kibarua na hivyo kuishia kwa ulevi
Wamehimiza ushirikiano wa serikali na makanisa na wanajamii kuwashughulikia vijana
By Linda Adhiambo