Biwi la simanzi limetanda katika mtaa wa Shinyalu Bar wadi ya Shieywe eneo bunge la Lurambi viungani mwa mji wa Kakamega baada ya ajuza mmoja wa miaka 80 kunajisiwa kabla ya kuwaua na mshukiwa mmoja kwenye nyumba yake nyakati za usiku.
Familia ya mwendazake ikiongozwa na nduguye kwa jina Simon Ojwang inasema kuwa marehemu Joyce Atieno alivamiwa usiku kwenye nyumba yake na mshukiwa mmoja anayedaiwa kutumwa na mwanamke mmoja ambaye mumewe ni mfanyikazi wa duka aliyekuwa akilalamika kuwa mumewe ana uhusiano wa kimapenzi na mjukuu wa ajuza huyo wa miaka 15 ambaye alikalia mtihani wa darasa la nane wa mwaka jana 2020.
Wanadai kuwa kabla ya marehemu kuwawa na kijana mshukiwa wa mauaji hayo alikuwa ametishia kumuua mjukuu wa ajuza huyo aliyemshuku kwa kufanya mapenzi na jirani mmoja wa duka japo alizuiliwa na nduguye marehemu Ojwang ambaye alimpata kwenye boma hilo.
Kwa sasa familia hiyo ambayo imekashfu mauaji hayo imeitaka serikali kuingilia kati kumnasa mwanamke huyo pamoja na mshukiwa wa mauaji hayo ambaye pia aliiba gesi ya kupika.
Wakati huo uo wenyeji wa mtaa huo wamelalamikia ukosefu wa usalama sehemu hiyo kwani usiku huo nyumba nyingi zilivunjwa na mali kuibiwa.
By Linda Adhiambo