Shinikizo zinazidi kutolewa kwa serikali kuu kutekeleza mapendekezo ya jopo kazi lililothathimini masaibu yanayokabili kilimo cha zao la miwa na ambalo liliongozwa na  gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya na waziri wa kilimo Peter Munya.

Seneta wa Kakamega Cleophas Malala ameelezea kughadhabishwa na hatua ya serikali kuu kuwekeza mabilioni kwenye sekta zingine na kufumbia macho masaibu wanayopitia wakulima wa miwa

Akizungumza katika eneo bunge Matungu, Malala ameitaka serikali kuu kutekeleza mapendekezo ya ropoti ya jopo kazi la miwa, akisema mapendekezo hayo yanalenga ufufuzi wa sekta hiyo

Malala aliyekua ameandamana na mbunge Peter Oscar Nabulindo amemtaka gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kuweka wazi zilikokwenda shilingi milioni 200 zilizotolewa na serikali yake kwa madhumuni ya kuwalipa wakulima wa miwa.

Kwa upande wake nabulindo amewataka wanasiasa eneo la Matungu kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kushirikiana naye kuwatimizia wakaazi ahadi alizowapa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo.

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE