Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha Eshisiru wadi ya Butsotso ya kati eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega baada ya familia ya Enock Irungu ambaye alikuwa afisa wa Dci kaunti ya Mombasa aliyefariki kutokana na mauaji ya gari alimokuwa ndani pamoja na maafisa wenzake kukanyaga bomu kule Lamu kupata habari ya kifo chake.
Familia hiyo ikiongozwa na babake marehemu Charles Mukoshi na mkewe Agnes Khayanje inasema kuwa walipata habari hizo za kifo cha mwanao kwa huzuni mkubwa.
Kulingana na wawili hao wanasema kuwa marehemu ndiye aliyekuwa tegemeo lao baada ya wao kustaafu huku wakiitaka serikali kuona kuwa wanapata haki ya kifo cha mwanao ikiwemo kutafuta suluhu la kudumu kumaliza kikundi cha Alshabaab kinachoendelea kuwaua wakenya wa tabaka mbali mbali wakiwemo maafisa wa usalama.
By Linda Adhiambo