Wakaazi wa eneo la Namutokholo eneobunge la Sirisia wana kila sababu ya kutabasamu baada ya serikali ya kaunti ya Bungoma kuzindua uchimbaji wa maji katika shule ya msingi ya Namutokholo D.E.B itakayosaidia kupigana na uhaba wa maji eneo hilo.

Akihutubu wakati wa kuongoza hafla ya uzinduzi wa mradi huo wa maji waziri wa huduma za umma katika serikali ya kaunti ya Bungoma Sabwami Keya amedokeza kuwa walifwata taratibu na sheria kabla kuafikiana kuanzisha mradi huo  ambao umetajwa kuwa wa manufaa tele.

Wakati uo huo Sabwami amempongeza gavana wa kaunti hii Wycliffe Wangamati kwa kuzidi kufanikisha miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali kaunti hii.

Naye afisa mkuu katika wizara ya maji kaunti hii bi Rosalia Soita akidokeza kuwa waliafiki kuanzisha mradi huo eneo la Namutokholo kutokana na uhaba wa maji eneo hilo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE