Serikali ya kaunti ya Kakamega inapania kutumia shilingi bilioni 16.158 kama makadirio ya mwaka wa kifedha wa 2021/2022 huku sekta ya afya ikitengewa shilingi bilioni 4.849 ambayo ni asilia 30% ya bajeti hiyo kutoka na janga la covid 19

Wakizungumza nje ya ukumbi wa mitano mjini Kakamega baada ya kutamatika kwa kikao cha kutoa maoni kuhusu bajeti hiyo, mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kaunti ya Kakamega Willis Opuka amesema waliafika kiwango hicho ili kuwezesha sekta hiyo kukabili janga la korona

Hata hivyo mwenyekiti huyo ameonekana kuitetea bajeti ya mwaka wa 2021/2022 kuwa hakuna miradi mipya itaanzishwa kabla ya kutamatika kwa ile iliyoanzishwa awali, hii ni baada ya swala la kutotamatika kwa baadhi ya miradi ambayo serikali ya kaunti hiyo imezindua hapo awali kuibuliwa na wakaazi wa kaunti hii, ikiwemo kutoanzishwa kwa ujenzii wa kiwanda cha majani chai katika eneo bunge la Shinyalu, kiwanda cha maziwa cha Malava na kiwanda cha mahindi katika eneo bunge la Lugari

Licha ya kuandaliwa kwa kikao hicho cha maoni kwa mjibu wa wizara ya afya, wananchi walionekana kughadhabishwa na waandalizi kwa kukosa kuvipeleka vikao hivyo mashinani kwa wananchi wote na kutojumuishwa kwa baadhi ya mapendekezo yao kwa bajeti hiyo…… Owen Musoma ni kiongozi wa vijana kaunti ya Kakamega

Kwenye makadirio ya bajeti hiyo, wizara ya kilimo imetengewa shilingi bilioni 1.61, wizara ya elimu shilingi bilioni 1.23, wizara ya barabara shilingi bilioni 1.34, bunge la kaunti ya Kakamega shilingi bilioni 1.16, afisi ya gavana shilingi milioni 292, wizara ya vijana, jinsia na michezo shilingi bilioni 1.37, wizara ya maji, mazingira na mali asili shilingi milioni 832 huku wizara ya fedha ikitengewa shilingi milioni 703

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE