Mshambuliaji wa England Harry Kane amesema anataka kuhamia Man City huku akiendelea kusukuma juhudi za kuondoka katika klabu ya Tottenham mwusho wa msimu
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaamini kwamba ana makubaliano ya mazungumzo na mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy kumuwacha aondoke mwisho wa msimu huu baada ya levy kumshawishi kusalia kwa msimu mmoja zaidi
Hatahivyo Man United iko tayari kumuuza mashambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial mwenye umri wa miaka 25, pamoja na mshambuliaji wa England Jesse Lingard – ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya West Ham kama njia ya kumleta Kane katika klabu hiyo
United huenda ikawasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Southampton na England Danny ings mwisho wa msimu ili kuimarisha safu ya mashambulizi ya mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer
By Samson Nyongesa