Waziri wa elimu wa humu nchini Profesa George Magoha kwa mara nyingine amewaonya wale ambao wanapia kujihusisha na udanganyifu wa mitihani ambayo inatarajiwa kuanza wiki kesho kwamba chuma chao kimotoni
Akizungumza katika shule ya msingi ya Kakamega mapema hii leo alipozuru shule hiyo kutathmini jinsi imejiandaa kufanya mtihani huo, Profesa Magoha amesema kuwa kama wizara hawatasita kuwachukulia hatua za kisheria wale ambao watapatikana huku akionya kaunti ya Homabay ambayo kwa sasa imo kwenye orodha ya kaunti ya migori na isipania ambazo zinagisiwa kujihusisha na udanganyifu huo
Waziri huyo vile vile amewatahadharisha baadhi ya wakuu wa shule ambao wanapanga kuwahamishia wanafunzi maeneo mengine ya kufanyia mtihani akidokeza kuwa wamewaka mikakati ya kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi ambaye alijisajili kufanya mtihani huo unaufanya huku akishikilia kuwa wako tayari kushughulikia changamoto za ugonjwa wa covid 19 shuleni iwapo zitatokea
Kuhusu swala la baadhi ya wakuu wa shule za kibinafsi kutowasajili wanafunzi kufanya mitihani hiyo, Magoha amesema watakabiliwa kwa mjibu wa kisheria
By Boaz Shitemi