Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF limesimamisha mechi zake zote za ndani kwa wiki mbili ili kuungana na watanzania katika maombolezo.
Aidha Kenya imehairisha mechi ya pili ya kirafiki dhidi ya Tanzania iliyopangwa kuchezwa Alhamisi hii jijini Nairobi.
Kocha JacobMulee,ameeleza kuwa mechi hiyo imesitishwa kufuatia kifo cha raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli.
Mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa sehemu ya maandalizi ya Kenya kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Misri na Togo zilizopangwa baadae mwezi huu.
Hayo yakijiri Kuna uwezekano mkubwa Cristiano Ronaldo, wa miaka 36, akarejea tena Manchester United kuliko Madrid akiamua kuondoka Juventus msimu huu.
By Samson Nyongesa