Kufwatia utata unaozidi kushuhudiwa kuhusu chanjo dhidi ya virusi vya CORONA kanisa la Redeemed Christian Center Kanda ya Magharibi sasa linaitaka serikali kutathmin upya chanjo hiyo kabla ya kuendeleza zoezi hilo
Askofu wa kanisa hilo Andrew Wafukho amesema kuwa yafaa zoezi hilo kusitishwa na ili chanjo hiyo idhibitishwe kuwa ni salama kwa afya kabla ya kuendeleza kutolewa kwa Wakenya
Kuhusu swala la BBI Wafuko amejiunga na wanaoshinikiza maafisa wa utawala wakiwemo machifu ma DO na makimisha wa kaunti kujiondoa kwenye zoezi hilo na badala yake kuwaachia Wakenya kupigia debe mswada huo
Askofu huyo amechukua Fursa hii kuwatakia wataihiniwa kote nchini kila laheri wanapoanza mtiani wao Wiki lijalo
By James Nadwa