Lubao FM | 102.2 Hz

Himizo kwa wenyeji wa kaunti ya Kakamega kuzingatia masharti ya corona

Siku moja baada ya waombelezaji kuzua vurugu kwenye hafla ya mazishi katika kijiji cha Shitirira wadi ya Butsotso Mashariki eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega wakimsuta naibu chifu wa sehemu hiyo Alex Mutende kushinikiza mwili wa marehemu Dauglas Kwatera aliyekuwa mhudumu wa bodaboda na kufariki kwenye ajali ya barabara kuzikwa mapema kufwatia agizo la rais Uhuru Kenyatta  kuthibiti msambao wa virusi vya corona,sasa mwakilishi wa wadi hiyo Mathews Nyangweso amewataka wenyeji kuzingatia masharti yaliyowekwa kuthibiti msambao wa virusi hivyo .

Akizungumza nje ya kanisa la PEFA la Elukaka wadi yake ya Butsotso Mashariki  , Yyangweso ametaja virusi hivyo kupanda kaunti ya Kakamega na kusema kuwa ipo haja ya wenyeji kuchukulia homa hiyo kwa uzito kwa kufwata masharti yaliyowekwa kuthibiti msambao wa virusi hivyo .

Kulingana na Nyangweso ametaja kuwa kwa sasa wadi maalum zilizotengewa waathiriwa wa virusi vya corona zimejaa na hakuna nafasi ya kuwahifadhi wagonjwa zaidi ikiwa watapatwa na homa hiyo.

By Linda Adhiambo

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE