Ni afueni kwa wakazi wa kaskazini mwa kaunti ya Kakamega haswa wa eneo bunge la Likuyani na Lugari baada ya tume ya huduma kwa mahakama nchini kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya kakamega kukubali kujenga mahakama eneo bunge la likuyani kama njia moja ya kuwasaidia wakaazi ambao wamekuwa wakisafiri mwendo mrefu kutafuta huduma hiyo katika mahakama ya mjini Kakamega.

Wakizungumza baada ya kikao na mawakili wa mahakama ya Kakamega cha kujadili utendakazi na changamoto wanazopitia mawakili hao mwenyekiti wa fedha na mipango katika tume ya huduma kwa mahakama Everline Olwanda amesema wanapania kujenga korti hiyo kwa manufaa ya wakaazi wa eneo hilo hii nii baada ya uongozi wa mawakili wa kaunti hii kulitaja kuwa changamoto kwao.

Mawakili hao wametaja upungufu wa majaji na hakimu, usalama na kucheleweshwa kwa mishahara yao kuwa changamoto kuu kwao swala ambalo tume hiyo kupitia kwa wanachama wamesema watalipa kipaumbele huku tume hiyo ikikiri kuwepo kwa upungufu kwa majaji humu nchini.

Naye gavana wa kakamega Fernandes Barasa amesema serikali yake itatenga shamba katika kila eneo bunge kuhakikisha mahakama inajengwa kila eneobunge ili kuhakikisha kila mkazi anapata huduma huo kwa karibu.

Habari naye Kefa Linda.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE