Familia 500 na wanafunzi 1500 kutoka jamii ya Lurambi wadi ya Butsotso Mashariki eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega wamenufaika na mradi wa maji kutoka kwa kampuni Moja ya Mchezo wa Bahati Nasibu kwa kima cha shilingi milioni 2.5
Mradi huu uliozinduliwa rasmi mapema leo katika shule ya msingi ya St Basil Lurambi unalenga kuisaidia jamii ya eneo hilo kupata maji safi ya matumizi kwa urahisi
Kulingana na meneja wa mauzo wa shirika hili Frank Ochieng, wanalenga kufikia jamii mia moja na miradi hii na ameitaka jamii hii kuulinda mradi huu ili uwasaidie
Meneja msimamizi Sasha Krneta ameeleza kuwa wanapania kuongeza usaidizi wao kwa jamii na huenda wakawapa wanafunzi madawati na Barakoa siku zijazo
Story by Boaz Shitemi