Ubabe wa uongozi wa muungano wa wauguzi kaunti ya Kakamega umeshuhudiwa huku mwenyekiti wa muungano huo tawi la Kakamega Eliud Molenje akifutilia mbali mgomo wa wauguzi hao naye katibu mtendaji wa muungano huo katika kaunti hiyo Renson Bulunya akishikilia kwamba mgomo ungalipo
Kulingana na mwenyekiti wa muungano huo tawi la Kakamega Eliud Molenje umedai kuwa wameamua kusitisha mgomo huo baada ya kuwepo na majadiliano na serikali ya kaunti hiyo ili kutoa huduma kwa wananchi wanaosumbuka matibabu kwa sasa
Ni uamuzi ulioungwa mkono na waziri wa afya wa kaunti ya Kakamega daktari Collins Matemba ambaye amesema kuwa utaratibu wa wauguzi hao kurejea kazini umewekwa na hakuna ambaye amepigwa kalamu jinsi ilivyoripotiwa awali
Hata hivyo katibu mtendaji wa muungano huo kaunti ya Kakamega Renson Bulunya amepuuzilia mbali uamuzi huo na kudokeza kuwa waliositisha mgomo huo wamehongwa kutoka kwa serikali kaunti hiyo na kuonya kuwa muuguzi yeyote ambaye atarejea kazini bila utaratibu wa kurudi kazini ambao umetiwa sahihi na katibu wa muungano ataelezea sababu za kuwa nje bila kufanya kazi na mwajiri anaweza kumwadhibu ni kauli ambayo iliungwa mkono na katibu mkuu wa muungano huo Seth Panyako
Story by Boaz Shitemi