Usimamizi wa shule ya msingi ya Nwikhupo katika eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega umelalamikia kutengwa kwa shule hiyo kwa kile wanachosema haijapokea fedha za serikali kupitia kwa wizara ya elimu za kufadhili elimu nchini licha ya shule zote kutoka eneo bunge hilo kupata mgao wao.

Wakizungumza na kituo hiki wakiongozwa naye Ronald Nabwera ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya shule hiyo,  viongozi hao wamedai kuwa tangu mwezi wa tisa mwaka jana hawajapokea fedha zozote kutoka kwa wizara ya elimu jambo wanalosema limechangia pakubwa katika kulemazwa kwa shughuli za masomo katika shule hiyo.

Hali sawia ikishuhudiwa katika shule ya msingi ya Kokoyo pamoja na ile ya Mukoko katika eneo bunge la Malava.

Aidha wanahoji kuwa juhudi zao za kutafuta usaidizi kutoka kwa afisi za elimu kaunti ndogo ya Malava hazijaweza kuzaa matunda na sasa wanaitaka serikali ya kitaifa kuingilia kati na kuwaokoa kutoka kwenye msiba huo.

Story by Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE