Wakulima wa mahindi kutoka eneo la Magharibi ya nchi wamepata afueni baada ya  kampuni ya utengenezaji mbolea ya Yara kuzindua mbolea aina ya Microp inayolenga kuongeza mazao pamoja na kutunza rotuba ya mchanga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbolea hiyo meneja wa kampuni ya Yara eneo la magharibi ya nchi Samuel Murono amesema tofauti na mbolea nyingine, mbolea ya Microp haitaathiri madini ya mchanga inapotumiwa.

Aidha amesema kampuni hiyo imeanzisha uhamasisho na wakulima ili kuwashawishi kukumbatia mbolea hiyo.

Uzinduzi huu unajiri msimu wa upanzi wa mahindi katika eneo la Magharibi.

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE