Familia moja kutoka kijiji cha Lwanza  eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega inalilia haki yao baada ya wao kugandamizwa na Bwenyenye mmoja eneo hilo anayesemekana kunyakua sehemu ya shamba wanaloishi bila idhini yeyote

Familia hiyo ikiongozwa na mama Beatrice Muyonga inaelezea kuwa tangu kufariki  kwa baba yao mzazi wamekuwa wakipitia changamoto duni kutoka kwa mkaazi mmoja eneo hilo anayedaiwa kuchukua baadhi ya kipande cha ardhi  wanamoishi kinyume na sheria jambo ambalo wanaelezea kuwa hali ya ufukara ambayo inawakumba inawasababisha  kupitia mateso na hali ngumu ya maisha

Aidha  kwa sasa wanaelezea kuwa wamejaribu kila wawezalo kurudisha ardhi  walioachiwa na baba yao ilhali hakuna matunda yoyote yameweza kuibuka.

Familia hiyo kwa sasa inaelezea kuwa hata baada ya wao kutii amri kutoka mahakama kuu ya Kakamega ya kufika mbele yake hakuna usaidizi wowote ambao wameweza kuona wala kupata tangu mwaka jana hadi wa leo jambo ambalo wanalitaka   ofisi za serikali zinazotetea maslahi ya binadamu kuingilia kati na kuona  kuwa mali  walioachiwa na baba yao inaregeshwa.

Haya yanajiri familia hiyo ikiitaka uchunguzi kufanyika kwa kina pale ambapo wanasema bwenyenye huyo anatoa habari za uongo dhidi yao ili kurithi kipande hicho cha ardhi

Story by Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE