Familia ya mzee Benard Orenga kutoka Nambale kaunti ya Busia  bado inalilia haki zaidi ya miezi kumi baada ya kudhulumiwa na maafisa wa polisi kutoka kituo cha Nambale.

Kwa mujibu wa mzee Orenga, polisi walimvamia yeye pamoja na familia yake ya watu kumi nyumbani kwake na kuwapiga hadi kuwajeruhi mnamo tarehe 30 mwezi machi mwaka uliopita kwa madai kuwa walikuwa wamekaidi amri ya kutopatikana nje wakati wa kafyu.

Kufuatia kisa hicho, mamlaka ya kuchunguza utendakazi wa polisi IPOA ilifanya uchunguzi dhidi ya maafisa 15 wa polisi na maafisa wengine sita wa kaunti ambapo walishtakiwa na afisi ya mkurungezi mkuu wa mashtaka ya umma kabla ya afisi hiyo tena kuyaondoa mashtaka dhidi yao.

Hatua hiyo ya kuwaondolea mashtaka maafisa hao wa polisi imeshtumiwa vikali na shirika lisilo la kiserikali la Haki Africa chini ya Mkurugenzi wake Hussein Khalid akisema uamuzi wa DPP umekiuka sheria.

Khalid aidha amewahakikishia waadhiriwa kuwa shirika hilo litaendelea kushinikiza kutendewa haki huku akionya polisi dhidi ya kukiuka sheria katika utendakazi wao.

Kesi hiyo iliyokuwa imewasilishwa mbele ya Jaji G.P Omondi wa mahakama ya Bungoma ilitupwa nje baada ya amri ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma DPP Noordin Haji kwa msingi wa kukosa ushahidi wa kutosha.

Story by Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE