Ukosefu wa heshima miongoni mwa viongozi wa kisiasa nchini ni kielelezo kinachotoa mfano mbaya kwa vijana hasaa wanafunzi
Ni kauli yake katibu mkuu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT tawi la Bungoma Ken Nganga akizungumza baada ya kuhudhuria hafla ya mazishi ya mama Mwanarabu Nawire Wangwe katika kijiji cha Mukangu eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamega.
Kulingana na katibu huyu, njia mwafaka ya kuwarekebisha wanafunzi inastahili kuafikiwa kwani pendekezo la kurejesha adhabu ya kiboko shuleni haliwezi fua dafu kikatiba.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na wakili ambaye pia ni mwanasiasa wa eneobunge hilo la Navakholo Edwin Wafula amabaye amesema kuwa kurejesha adhabu ya kiboko shuleni itakuwa kinyume na sheria za nchi.
Wakili Wafula amelaumu viongozi walioko mamlakani kwa kukiuka kipengee cha 6 kwenye katiba kwa kukosa maadili katika mikutano ya hadhara na kusema huenda ndio huchangia ukosefu wa nidhamu pia kwa wanafunzi shuleni
Wazazi ambao pia ni walimu wastaafu kutoka eneo hilo la Navakholo wamewataka wazazi kuajibikia nidhamu ya watoto wao na wala si kuachiwa walimu tu shuleni..
Story by Imelda Lihavi