Wanafunzi 12 wa shule ya upili ya wavulana ya Ingotse iliyoko eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamega ambao wanashukiwa kujaribu kuteketeza bweni lao watasalia kwenye Rumande za jela la Kakamega baada ya kufikishwa kwenye mahakama ya Kakamega na kushtakiwa na kosa la kujaribu kuteketeza bweni lao.

Washukiwa hao 12 walifikishwa kwenye mahakama ya Kakamega siku ya jumanne na mbele ya Hakimu mkuu mwandamizi Erick Malesi na kusomewa mashtaka ya kujaribu kuteketeza bweni lao wakitumia mafuta ya petroli.

Hata hivyo wanafunzi hao wote 12 walikanusha mashtaka dhidi Yao na kuamriwa watatu wao ambao Wako Chini ya miaka 18 kupelekwa kwenye Rumande za watoto ya Kakamega huku 9 ambao Wana zaidi ya umri wa miaka 18 kupelekwa kwenye Rumande za jela la Kakamega Hadi tarehe 15/2/2021 ambapo kesi dhidi yao itakapoanza kusikizwa.

Hata hivyo Hakimu huyo aliamrisha sampuli za damu ya Washukiwa hao kuchukuliwa na kuasilishwa Kwa mahabara kuu ya serikali na ripoti ya sampuli hiyo pamoja na vyeti vya kuzaliwa vya wanafunzi hao kuasilishwa mahakamani siku hiyo .

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE