Serikali imetakiwa kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha mikasa ya moto shuleni ambayo inaendelea kushuhudiwa  katika shule nyingi humu nchini hasa kaunti ya Bungoma ambapo mkasa wa hivi punde umekumba shule ya upili ya marafiki ya Kimabole ambapo wanafunzi kumi na watatu wa shule hiyo wametiwa nguvuni kwa kudaiwa kuhusika katika uteketezaji wa maabara shuleni humo.

Akihutubu baada ya kuzuru shule ya upili ya marafiki ya Kimabole eneobunge la Mlima Elgon ambayo maabara yake iliteketea usiku wa kuamkia leo, mwenyekiti wa muungano wa wazazi kaunti ya Bungoma Nyongesa Watulo amesema ni sharti serikali ichukulie swala hilo kwa uzito na kuwataka wanafunzi kujiepusha na visa hivyo.

Aidha watulo amesema anaunga mkono matamshi ya waziri wa elimu profesa George Magoha ya kutaka wanafunzi ambao wamechangia kuteketeza shule kutoruhusiwa katika shule nyingine.

Baadhi ya wazazi wa shule hiyo ya Kimabole wakisimulia  masaibu waliopitia katika juhudi za kuuzima moto huo na wanafunzi wakiruhusiwa kwenda nyumbani kwa muda usiojulikana.

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE