Takriban ya wanafunzi 12 wa shule ya wavulana ya Ingotse eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamega wanazuiliwa katika kituo Cha Navakholo baada ya jaribio lao la kuteketeza bweni kutipuka usiku wa kuamkia leo.
OCPD wa Navakholo Richard Omanga amehoji kuwa washukiwa hao walitiwa mbaroni huku wakipatikana na mafuta ya petroli lita tano ndani ya bweni lao.
Omanga amesema hiki ni kisa cha pili ambapo wiki mbili zilizopita wanafunzi wa shule ya upili ya Burangasi walijaribu kuliteketeza bweni lao.
Story by By Imelda Lihavi