Kizahazaha kimeshuhudiwa katika soko la Malava lililoko eneo bunge  hilo Kaunti ya Kakamega baada ya msichana mwenye umri wa miaka 19 kwa majina Anjelina Alima kupatikana akitaka kumgawa mwanawe mchanga mwenye umri wa miezi 4.

Kulingana na mwanaharakati wa haki za watoto eneobunge la Malava  Kenedy Shikuku  amehoji kuwa msichana huyo alipachikwa mimba na kijana mwingine ambaye alimruka jambo lililo pelekea afikie  hatua ya kugawa mtoto huyo

Aidha Shikuku amesema kuwa licha ya kwamba wamemurudishia mtoto huyo huenda akamuuzia mwanamke mwingine ambaye anashukiwa kuwa mtekaji wa watoto eneo hilo. Hata hivyo Shikuku ametumia fursa hiyo kuwaonya watoto wachanga dhiti ya kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi wakiwa wachanga kuwa itawaadhiri baadaye

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE