Serikali ya kaunti ya Kakamega imetakiwa kutoa idadi kamili ya walemavu ambao wamedhulumiwa kijinzia ili wadau wanaoshugulikia haki za walemavu nchini wachukuwe hatua ya kuhakikisha kuwa visa hivyo vinapungua.
Ni kauli iliyotolewa na mwenyekiti wa walemavu katika kaunti ya Kakamega Lucy Mulombi baada ya mafunzo yalioandaliwa mjini Malava ambaye amehoji kuwa visa hivyo vimeongezeka kutokana upepetevu wa maafisa wanaostahili kushugulikia maswala hayo.
Mulombi pia amesema kuwa walemavu wengi hasa wasichana wameshindwa kuwakilishwa vyema wakati wanawasilisha kesi yao katika kituo cha polisi ama hosipitali kwa kisingizio cha ukosefu wa ushahidi.
Kulingana na mtetezi wa haki za binadamu eneo bunge la Malava Boaz Mukaramoja amewataka walemavu hao kuripoti visa vyoye vya dhuluma ambavyo vinashuhudiwa ili washugulikie kwa wakati unaofaa.
Aidha afisa wa kliniki katika hosipitali ya Malava Madilto Ambale amewahimiza walemavu hao kujitokeza kwa wingi na kuripoti hosipitalini ili waweze kusaidika.