Aliyekuwa mbunge wa Teso Kusini Mary Emase amewataka magavana nchini kufanya mazungumzo na madaktari na wahudumu wa afya wanaogoma ili warejee kazini.
Akihutubu kwenye hafla moja katika eneo la Segero kaunti ndogo ya Teso Kusini Kaunti ya Busia, Emase amasikitika kuwa wananchi wengi ambao hawana uwezo wa kupata huduma za matibabu katika hospitali za kibinafsi wanaendelea kuumia kutokana na mgomo huo.
Kwa upande wake mbunge wa eneo hilo Geoffrey Omuse amemtaka gavana wa kaunti ya Busia Sospter Ojaamong kuimarisha sekta ya afya anayosema imo katika hali mbaya.
Omuse kadhalika amemtaka gavana Ojaamong kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuwapiga jeki wakulima hasa msimu huu ya upanzi.
Hata hivyo gavana Ojaamong amelalama kuwa fedha ambazo kaunti ya Busia hupokea kutoka kwa serikali ya kitaifa hazitoshelezi mahitaji ya sekta ya afya ingawa ameahidi kuweka mikakati ya kuboresha sekta hiyo.
Story by Hillary Karungani