Idadi kubwa ya wanafunzi hasa wavulana bado hawajarejea shuleni licha ya shule kufunguliwa rasmi zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya wazazi katika shule ya upili ya Wabukhonyi katika eneo bunge la Webuye Mashariki kaunti ya Bungoma Job Chelongo, idadi kubwa ya wanafunzi wa kiume hawajarejea shuleni, wengi wao wakijishughulisha na vibarua mitaani.
Chelongo sasa amewataka wazazi na asasi za serikali kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanarejea shuleni, akiongeza kuwa tayari baadhi ya wanafunzi wamepewa ufadhili wa elimu licha ya wao kuwa nyumbani.
Usemi wake unajiri wakati ambapo kamishna kaunti ya Bungoma Samuel Kimiti, ametoa ilani ya kuwatia mbaroni wazazi ambao wanao hawajarejea shuleni kufikia sasa.
Story by Hillary Karungani