Hali ya huzuni Imetanda katika mji wa Kanyandiri eneo kuu la Sakwa eneo la kaunti ya Bondo ambapo mwanamume wa miaka thelathini amekamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Bondo baada ya kudaiwa kumnajisi mpwa wake wa miaka tisa.

Mtuhumiwa ambaye anajulikana kama Lukas Wata alishikwa na familia yake na kumpeleka katika kituo cha polisi siku ya Jumanne usiku.

Kulingana na kaimu mkuu wa eneo kuu la Sakwa Bwana. William Oreme, inasemekana kuwa mshukiwa alishawishi watoto watatu kumfuata ndani ya nyumba yake kabla ya kumnajisi.

Anahutumiwa pia kumpiga mtoto huyo wakati alijaribu kupiga kelele kuomba msaada.

Maneno ilitoka baada ya mdogo kutoroka na kuripoti suala hilo kwa mjomba wake.

Msimamizi alimwaambia kituo kimoja cha humu nnchini  kwamba mdogo huyo alitibiwa katika hospitali ya Nango na baadaye kupelekwa katika hospitali kuu ya Bondo kwa matibabu zaidi

Wakati huo huo mchakato wa mashtaka umeanza na mshukiwa kuzuiliwa katika kituo cha polisi .

By Winnie Akinyi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE