Kulingana na baraza la magavana,serikali, za kaunti zitalazimika kufungwa.ifikiapo tarehe ishirini na nne mwezi wa sita mwaka wa elfu mbili ishirini na moja kabla wizara ya uwekezaji kulipa shilingi bilioni mia moja na mbili nukta sita wanazomiliki.
Huku akihutubia umma,naibu wa kamati la magavana bwana Martin Wambora siku ya Jumatatu aliilaumu wizara ya uwekezaji kwa kutowajibika ipasavyo kikatiba.
Wambora ambaye pia ni gavana wa Embu alisema kuwa wizara ya uwekezaji bado haijawalipa pesa hizo ilihali zimesalia wiki mbili tu kufika mwishoni mwa mwaka wa kifedha.
Gavana Wambora alisema pia hali hii imechangiwa na matakwa ya serikali za kaunti malipo yaliyopangwa kwa ajili ya mwaka wa kifedha wa kati wa elfu mbili ishirini na ule wa ishirini na moja ulioafikiwa na wizara ya uwekezaji na kuidhinishwa na seneti kulingana na kauli ya usimamizi wa umma wa fedha .
Wambua alisema kuwa pesa hizo bilioni mia moja na mbili nukta sita zimegawika ifwatavyo;bilioni tatu nukta tano zafaa kulipa kaunti ya Nairobi kama salio la mwaka wa kifedha waelfu mbili kumi na tisa hadi ule waelfu mbili ishirini na ishirini .shilingi bilioni mbili nukta tatu zafaa pia kulipa kaunti ya Nairobi ambazo zilifaa kutumika januari na bilioni moja nukta nne ambazo ni za februari
Shilingi bilioni kumi na nne nukta nne yafaa kulipa kaunti ishirini na tano kwa minajili ya mwezi wa tatu huku ishirini na nane nukta tano ikilipwa kwa kaunti kumi na saba kwa ajili ya Aprili,bilioni ishirini na tano nukta tatu kwa mwezi wa tano na mwisho bilioni ishirini na sita nukta tisa kwa mwezi wa sita..
By Mary Owano