Rais Uhuru Muigai Kenyatta amewaongoza wakenya  kuomboleza aliyekua mbunge wa Gem Wasghington Jakoyo Midiwo aliyefariki siku ya Jumatatu jioni.


Mwendazake Midiwo, aliongoza eneo bunge la Gem kama mbunge kwa miaka mitatu kutoka mwaka wa elfu mbili kumi na mbili hadi mwaka elfu mbili kumi na saba kwenye chama cha kitaifa National Rainbow Coalition (NARC) na chama cha Chungwa Orange Democratic Movement(ODM) huku akiwa ameaga na umri wa miaka hamsini na nne.


Kutokana na habari kwa familia,marafiki pamoja na wafuasi wa Midiwo, Rais Uhuru Muigai Kenyatta amemwomboleza huku akisema kwamba alikua mwanasiasa shupavu na alijitokeza na kusema ukweli kila siku.


”Nimepata ujumbe mfupi kuhusu kifo cha rafiki yangu, Mweshimiwa Jakoyo Midowo kwa mshtuko na kutoamini, nilikua na yeye hivi karibuni eneo la Nyanza tukizindua miradi eneo lake la zamani kama mbunge,” Rais alikumbuka.


Rais alisema kwamba mwendazake Jakoyo alikua mkamilifu kwa mjadala wa bunge kuhusu jambo la umuhimu kwa sirikali na pia kutetea Wakenya.
Kando na kazi ya siasa mwendazake Jakoyo aliyojitokeza kwa baadhi ya runinga humu nchini huku akizungumzia vitu vinavyo wadhuru wananchi.
BY WINNIE AKINYI

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE