Mara nyingi akina mama hujifungua watoto tatu au wawili safari moja.Lakini mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi Bill Kalumi, kutoka hospitali ya taifa ya Kenya amesema:”Mara nyingi hali hii hutokea iwapo mtu ametumia tiba ya uzazi.”

Lakini hali hii hutokea sana barani Afrika wakati ambao mwanamke anaanza kutumia dawa za homoni ambazo ni kama za kuzuia kupata ujauzito.Hii inaweza kumchukua muda kwa kipindi cha kutungwa mimba, Dkt Kalumi anaeleza.

Hivyo matokeo yake yanaweza kuwa mayai mengi badala ya moja wakati wa mzunguko wa mwanamke kwa mwezi.Uzazi wa watoto wengi kwa pamoja, ni jambo la hatari kwa mama na watoto.

Mara nyingine baada ya kufanya vipimo vya picha, inashauriwa kupunguza idadi ya watoto waliopo tumboni.Watoto kuzaliwa wengi wako kwenye hatari ya kupata maambukizi.Kwa huyu mama aliyejifungua watoto 10 hivi karibuni, Daktari anasema Sithole yupo kwenye hali nzuri.

Gosiame Thamara Sithole alijifungua kwa njia ya upasuaji wakati mimba ikiwa na wiki 29 , huko Pretoria Jumatatu jioni.Dawa za kisasa tayari zinaruhusu wanawake kujifungua watoto umri ukiwa umeenda tofauti na wakati wa mababu zetu.

By Marseline Musweda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE