Maafisa wa polisi eneo la Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon wanamzuilia mwanamume mmoja kutoka kijiji cha  kaptoka  anayedaiwa kumpiga kisha kumuua mwanawe Geofrey Kisiero mwenye umri wa miaka ishirini na nane kwa madai ya kuiba gorogoro tatu ya mbolea na kuiuza.

Kulingana na chifu wa kata ya Sasur,  Jackson Komon mwanamume huyo Moses Kisiero ambaye ni naibu chifu mstaafu wa kata ndogo ya Toroso, anadaiwa kumpiga mwanawe na kupelekea kifo chake mwendo wa saa saaba  usiku baada ya kudaiwa kuiba gorogoro tatu za mbolea siku chache zilizopita kisha kuiuza.

Wakati uo huo Komon amedokeza kuwa Kisiero alihusika kwenye mzozo wa kinyumbani na mkewe mchana kabla tukio hilo la mauaji kutendeka usiku wa kuamkia leo.

Amedokeza kuwa unywaji wa pombe huenda ulichangia kisa hicho na kuwataka wazazi kuwekeza kwenye elimu ya wanao huku mwili wa mwendazake ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhi wafu kwenye hspitali ya Dreamland mjini Kimilili.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE