Wakaazi wa eneobunge la Mlima Elgon na kaunti ya Bungoma kwa jumla wamehimizwa kujiunga kwenye chama cha United Democratic Aliance (U.D.A) ambacho kimetajwa kuwa cha kuunganisha wananchi kando na kujali maslahi ya mwananchi wa kawaida.

Akihutubu mjini Cheptais baada ya kuzindua usajili wa wananchama wa U.D.A eneobunge la Mlima Elgon mbunge wa eneo hilo Fred Kapondi, amewasihi wakaazi kujisajili kwenye chama hicho ambacho anasema kina umaarufu miongoni mwa wananchi huku ajenda yake ni kuwajibikia maslahi ya mwananchi wa kawaida.

Kwa upande wake mratibu wa chama cha U.D.A kaunti ya Bungoma mhandisi Mike Malomba akidokeza kuwa tayari wametoa mafunzo kwa makarani wa viwango mbalimbali  huku idadi ya wananchi wanaojisajili ikizidi kuongezeka.

Wakati uo huo Malomba amehoji kuwa chama hicho kitahakikisha mwananchi wa kawaida anapewa kipaumbele.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE