Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo mshukiwa wa wizi wa ng’ombe ameuawa kisha kuteketezwa na wakaazi waliokuwa na hasira kwenye soko la Namutokholo eneobunge la Sirisia mapema leo huku mwingine akiokolewa na maafisa wa polisi japo akiwa hali mahututi.

Kulingana na Alex Wafula mkaazi wa Chebich eneobunge la Mlima Elgon  aliamshwa na babake mkwe usiku wa manane kufahamishwa kutoweka ng’ombe wake zizini na baada ya ushirikiano waliweza kuwakamata washukiwa wawili eneo la Namutokhkolo wakimsafirisha ng’ombe huyo kuelekea soko la Sirisia.

Aidha wafula anasema licha ya maafisa wa utawala kuwataka wakaazi kuwatambua washukiwa wa wizi,  imekuwa vigumu kwao kuripoti washukiwa hao kwa afisi husika.

Waathiriwa wa wizi wa mifugo eneo la Namutokholo wanasema walichukua hatua ya kumteketeza mshukiwa huyo ili kuwa funzo kwa wezi wengine.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE