Viongozi wa ANC eneo bunge la Lurambi wanaitaka serikali kuona kwamba mikopo inayochukuliwa kwa ajili ya janga la corona inawafaidi wakenya mashinani
Wakiongea katika wadi ya Butsotso Mashariki kupitia kwa mwenyekiti Musa Rajab wamesikitikia kiwango kikubwa cha ubadhirifu serikali huku wakenya wakisumbukana kiuchumi.
Rajab amewataka wakenya kumuunga mkono kinara wa ANC Musalia Mudavadi kama kiongozi pekee mwenye tajriba ya kufufua uchumi
Kiongozi wa akina mama katika chama cha ANC eneo la Lurambi Ruth Ombayo ameitaka wizara ya afya katika serikali ya kaunti ya Kakamega kutoa chanjo ya corona kwa usawa bila kuwabagua wananchi
Bi Ombayo vile vile amewataka wakenya kuzingatia magizo ya afya kuepusha msambao wa virusi vya corona
Wakati uo huo bi Ombayo amewataka wagombea wa nyadhifa za uongozi kupitia chama cha ANC kudumisha amani huku akiwahakikishia haki katika zoezi la mchujo
By Linda Kefa