Wenyeji wa kijiji cha Bulovi wadi ya Isukha Kaskazini eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega wamebaki vinywa wazi na kushikwa na butwaa baada ya ng”ombe wa David Mateche kujifungua yai badala ya ndama.

Kulingana na mwenye ng’ombe huyo David Mateche anasema kuwa ng’ombe wake alianza kuonyesha dalili za kuzaa jioni na kujifungua yai hilo badala ya ndama jambo ambalo lilimfanya kushikwa na butwaa akidai kuwa ni mazinga umbwe.

Ni kisa ambacho kiliwaacha wenyeji vinywa wazi wakisema kuwa hawajawai kushuhudiwa ng”ombe akijifungwa yai huku baadhi yao  wakihoji kuwa huenda kulikuwa na ihusiano kati ya ng’ombe huyo na jogoo ndiposa akazaa yai.

Kwa upande mwingine wazee wa jamii hiyo wakiongozwa na Peter Mateche Muluka wameamua kufanya tambiko kwa kufwatana na mila na desturi ya jamii hiyo kupitia kwa dawa za kienyeji kisha wamuuze ng”ombe huyo kuondoa misimu katika familia hiyo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE