Hali ya majonzi imetanda katika kijiji cha Ingusi kata ndogo ya Eshikalame wadi ya Musanda eneo bunge la Mumias Magharibi kaunti ya Kakamega baada ya mama wa miaka 62 kupigwa na radi hadi kufariki papo hapo wakati mvua ilipokuwa ikinyesha.

Kulingana na Jackson Muramba ambaye ni mumewe marehemuRrosemary Muramba amedokeza kuwa mkewe alikumbana na mauti yake alipokuwa akielekea jikoni kuanda chakula cha jioni .

“Mke wangu alitoka kwa nyumba kubwa na alikua akienda jikoni kupika chakula ya jioni na mvua ilikua inanyesha. sasa nilisikia radi ikipiga na hiyo radi ikipiga ikupiga kama ya kawaida nilishtuka na nikaamua kutoka nnche. Sasa mimi kutoka nnche nikapata mke wangu amepigwa na radi na amefariki.”

Kwa upande wao wanyeji wa maeneo hayo wanasema kuwa sio kisa cha kwanza kutokea sehemu hiyo kwani watu wengi wamepoteza maisha yao kwa kupigwa na radi.

Naibu chifu wa Eshikalame Sarah Kayore amethibitisha mkasa huo na kuwarai wenyeji kuwa waangalifu haswa msimu huu wa mvua.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE