Hali ya simanzi imetanda katika kijiji cha muraka kata ya ilesi eneo bunge la shinyalu baada ya mwili wa aliyekuwa mkuu wa nyumba kumi katika kata hio kupatikana ameaga kwa njia tatanishi
Kulingana na majirani walioshuhudia, mwili wa richard khayumbi ulipatikana mapema hii leo kitandani mwake huku mwili wake ukiwa umechanika na kutoa harufu mbaya. Inakisiwa kuwa khayumbi alionekana siku ya jumapili kwa mara ya mwisho
Hali hio ya taharuki imewashangaza wakaazi huku wakiomba serikali kuingilia kati kwani wanahofia usalama wao ikiwa mkuu wa nyumba kumi anaweza kuangamia kwa njia kama hio
Akidhibitisha kisa hicho, mkuu wa nyumba kumi kaunti ndogo ya shinyalu hussein muhanji amesikitikia kisa hicho huku akikisi kuwa khayumbi aliuawa na watu wasiojulikana kufuatia msako walioufanya juzi wa majambazi katika kata hio
Hata hivyo, muhanji alisisitiza kuwa hao kama nyumba kumi hawatarudi nyuma katika kuwaekea usalama wakaazi wa eneo hilo
Story by Tomcliff Makanga