Mwendeshaji mmoja wa bodaboda kaunti ya meru anatafutwa na idara ya upelelezi wa jinai DCI kwa minajili ya kumbaka mschana wa umri ya miaka minane jana.
Idara hiyo ya upelelezi inasema kuwa katika bunge la Igembe Kusini, eneo la Baibariu, mshukiwa huyo alimbebamschana huyo kumPeleka nyumbani kwao lakini walipokuwa njiani mshukiwa huyo alibadili mkondo na kwenda nyumbani kwake ambako alitekeleza uovu huo.
Kupitia ukurasa wa Twitter wa idara hiyo inasema kuwa mshukiwa huyo baadaye alimpeleka mtoto huyo nyumbani kwao kabla ya kutoweka.
Msichana huyo anatibiwa kwenye hospitali moja ya eneo hilo huku msako dhidi ya mshukiwa huyo ukiendelea.
Shirika hilo la kukabiliana na uhalifu limetoa wito kwa wakazi ambao huenda wanafahamu aliko mshukiwa huyo wawasilishe habari kwa polisi bila kujitambulisha kupitia nambari 0800722203 isiyotozwa ada.