Mbunge wa Likuyani daktari Enoch Kibunguchy amemtahadharisha naibu rais William Ruto kujitenga na kinara wa ODM Raila Odinga hii ni kufuatia tetezi kuwa wawili hao wananuia kubuni muungano mbele ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Kwenye mkao na wanahabari katika eneo bunge lake, Kibunguchy amehoji kuwa kinara wa ODM Raila Odinga si kiongozi wa kuaminika kuweka mkataba wa kisiasa naye, kwa kile amedai kiongozi huyo amekuwa na hulka ya kuwatumia viongozi wengine na mwishowe kuwatema.
Kufuatia repoti ya mkaguzi mkuu wa serikali nchini Nancy Gathungu, kutokana na matumizi mabaya ya fedha zilikuwa zimenuiwa kuzuia msambao wa virusi vya korona katika kaunti mbalimbali za humu nchini, sasa Kibunguchy ametaka kaunti ya Kakamamega kuelezea namna jinsi fedha hizo zilivyo kadiriwa .
Mbali na hayo kwa mara ya kwanza Kibunguchy amekubaliana na usemi wake gavana Wycliffe Oparanya kufuatia matamshi yake ya kutaka fedha zilizo kuwa zimetengwa kutumika kwenye kura ya maoni ya kubadilisha katiba kupitia ripoti ya BBI , kutumia fedha hizo kukabiliana na maambukizi ya virusi vya korona, huku akiunga mkono azima ya Oparanya kupigania kiti urais ifikapo mwaka ujao , kwa kile alisema hiyo ndo hadhi yake Oparanya, na kumtaka gavana huyo kujitenga na swala kupigania kiti bunge katika eneo na Butere na Likuyani mtawalia.
By Richard Milimu