Mabingwa wa Ufaransa klabu ya Paris St-Germain wamefanya mawasiliano na wawakilishi wa mshambualiaji nyota wa Liverpool Mohamed Salah Mwenye umri wa miaka 28, ili kumsajili mchezaji huyo tegemezi pia wa timu ya taifa ya Misri.

Huku kocha wa PSG Mauricio Pochettino pia amewasiliana na mshambuliaji nyota wa Tottenham na timu ya taifa ya England Harry Kane mwenye umri wa miaka 27, kuhusu uwezekano wa nyota huyo kuhamia Ufaransa. 

Hayo yakijiri Miamba ya soka nchini Ujerumani klabu ya Bayern Munich itajaribu kumsajili kocha wa Liverpool Jurgen Klopp mwishoni mwa msimu endapo kocha wao Hansi Flick ataenda kuitumikia timu ya Taifa ya Ujerumani. 

Timu ya Chelsea na PSG ilijikatia tikiti ya kuwania Kombe la klabu bigwa barani Ulaya huku leo ikiwa ni zamu ya Liverpool na Manchester city ambapo Real watachuana na Liverpool huku Man City wakichuana na Borussia Dotmond

By Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE