Serikali ya kaunti ya Kakamega kwa ushirikiano na mashirika ya ufadhili imetoa vifaa kwa wakulima kuendeleza ufughaji wa samaki kama njia ya kutosheleza lishe
Akiongea baada ya kupokea vifaa hivyo mshirikishi wa mradi huo Noman Munala amesema vifaa hivyo vitakabidhiwa wakulima siku ya Alhamisi kaunti inapoadhimisha siku ya Samaki eneo la Eshisiru Lurambi akisema ni njia ya kuendelea kuwahimiza wakulima kukumbatia kilimo cha samaki
Munala amewataka wakulima kujitokeza kupata mafunzo na kuweza kukumbatia kilimo cha samaki ambacho kwa sasa kinapata ufadhili unaostahili kutoka kwa serikali na mashirika ya wafadhili
By Linda Adhiambo