Serikali ya kaunti ya Kakamega inaimizwa kuimarisha juhudi zake za kukusanya ushuru katika soko ili kuimarisha miundo msingi katika. Ukusanyaji wa ushuru unasaidia kaunti hio kuendeleza shughuli mbalimbali katika kaunti hio.
Wachuuzi wa ngombe katika katika kaunti wakiongozwa na Nyayo Shivambo, wanawaomba wakusanyaji ushuru kutembelea soko la Nambacha, kaunti ndogo ya Navakholo ambayo wachuuzi hao wanasema kua ni muda mrefu wanafanya biashara yao bila kukata risiti ambazo kwa kiasi kikubwa huwasaidia kukadiria biashara yao.
Shivambo vilevile amesema kua wizi wa mifugo umekithiri kiasi kua wanapojihusisha na biashara yao wanahofia kujipata katika mikono mibaya ya serikali. Anawaomba wachuuzi wenzake kufuata taratibu zifaazo wanaponunua ngombe.
Naye mzee wa mtaa kutoka kata ndogo ya Samitsi, eneo bunge la Malava, Charles Chimuche anawaimiza wakaazi wa eneo hili kutumia mvua kubwa inayoyesha kujihusisha kwa ukulima ambayo utawafaa siku za usoni.
Mzee Chimuche anafurahia utulivu ulioko baada ya kuwepo visa kadhaa vya wizi siku chache zilizopita na pia ametumia fursa hio kuwaonya vijana wanatembea kijijini humo na kuwasumbua wananchi haswa wakati wa usiku.
By Wycliffe Andabwa