Shirika la PIMAC likiongozwa na Pius Maasai Mwachi mkurugenzi mkuu anayesimia malipuko ya majanga KV Moto, ajali na mengine kama haya kwa lugha ya kimombo Disaster Emergency wametumia siku ya Madaraka kutoa mafunzo kwa wenyeji wa Eshisiru eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega ya jinzi ya kukabiliana na haya majanga.
Mwachi amesema kuwa kutakua na uchaguzi wa viongozi ambao watahakikisha kwamba wametembelea vijiji mbalimbali kwa huo mradi wakiongozwa na wanaosimamia wadi mbalimbali nakupanga mipango kabambe ya kuwasaidia wakenya kiujumla
Amesema kuwa ajali za moto na za barabara zimekua mingi kwa hivyo kutakuwepo na Patron atakaye saidia vilabu viwe na nguvu akishirikiana na viongozi wengine
Hatahivyo Samwel Oketch chifu anayewakilisha wadi ya Butsotso Kusini pamoja na OCPP wa Eshisiru Abdul Hassan wameunga mkono shirika hili na kutembea kwa pamoja ili kuakikisha kuwa wananchi wanasaidika. Samwel alisema kuwa wataendelea kutembea ili waweze kuongea na wananchi na kuwapa mafunzo
By Lindah Adhiambo