Wakaazi wa soko la Kaunda kwenye wadi ya Bunyala eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamega wamehakikishiwa uimarishaji wa usalama sehemu hizo baada ya kikao cha pamoja na vigogo wa kiusalama wa eneo hilo

Wakiongozwa na naibu kaunti kamishna wa Navakholo Geoffrey Tanui amesema usalama unaanza wa mwanainchi wa kawaida na kuwahakikishia usalama wa kutosha kutoka kwa maafisa wa usalama baada ya kupata nyumba za maafisa wa usalama na kusema wataharakisha kuleta maafisa wa usalama wa kutosha

Naye kamanda wa polisi eneo bunge la Navakholo Gabriel Muriu akitilia mkazo semi hizo na kuwataka wanainchi wa sehemu hizo kuimarisha ushirikiano mwema na maafisa wa usalama

Naye mwakilishi wadi wa Bunyala Magharibi Edward Namunyu Masinde akiwataka wakaazi wa sehemu hizo kutomuwa na wasiwasi baada ya swala la usalama kupewa kipau mbele huku akielezea mipango kabambe ya maendeleo kwenye wadi hiyo

By Ernest Luvisia

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE