Wakazi wa Maella huko Naivasha walishtuka baada ya mume aliyedharauliwa kwenda kwa hasira na kumchoma mkewe kisu zaidi ya mara 15,na kumua papo hapo. Mwanaume huyo alitoroka wakati wa kisa cha jumatatu asubuhi kabla ya umma kumshika.

Mwathiriwa alikuwa pamoja na shangazi yake katika eneo lenye utajiri wa kilimo wakati mshukiwa alimshambulia. Shahidi,Solomon Muturi,alisema mtuhumiwa huyo aliongea na mke mbali na shangazi yao kabla ya kumgeuka.

“Alikuwa amekuja kumshawishi mke arudi nyumbani lakini baada ya kukataa ofa zake alimdunga kwa kisu zaidi ya mara 15 kabla ya kukimbia .”alisema

Alisema kuwa mwathiriwa alitokwa na damu mingi na alikufa wakati watu wa umma walifanya juhudi za kumkimbiza hospitalini.

kwingineko Mwakilishi wadi wa Lakeview Simon Wanyoike alisema kulikuwa na harufu kutoka nyumbani kwake na ilikua kiashiria mtu amefariki. chanzo cha kile kinachoweza kumua mwanamke huyo wa makamo hakijulikani.OCPD wa Naivasha Samuel Waweru amedhibitisha visa vyote viwili,akiongeza kuwa mshukiwa wa kesi ya mauaji alikuwa amekamatwa.

“Mshukiwa atashtakiwa kwa mauaji wakati kesi ya pili tunasubiri postmortem kujua sababu ya kifo,”alisema

By marseline musweda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE