Shinikizo zinazidi kutolewa kwa wawakilishi wadi kwenye bunge la kaunti ya Bungoma kushiriki mazungumzo ya kina na gavana wa kaunti hii Wycliffe Wangamati ili kusitisha malumbano ambayo yanaendelea kushuhudiwa kwa sasa.

Kulingana na kamishna katika kanisa la Jeshi la Wokovu tawi la Kenya West Stephen Chepkurui ipo haja kwa wawakilishi wadi kwenye bunge la kaunti hii, kuzika tofauti zao na kufanya kazi kwa karibu na gavana Wangamati  ili kufanikisha ajenda ya maendeleo kwa wananchi

Wakati uo huo Chepkurui amewataka wawakilishi wadi hao kusitisha pendekezo la kutaka kumng’atua afisini gavana Wangamati, kando na kuwasihi vijana kuwaepuka wanasiasa wenye nia ya kuwatumia vibaya.

Kwa upande wake Meja Haron Chepsiri kamanda wa divisheni katika kanisa hilo tawi la Bungoma akiwashauri vijana kujiepusha na matumizi ya mihadarati,  ambayo imetajwa kuwa hatari kwa afya yao.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE