Wimbi la mgomo shuleni limeshika shule nne katika kaunti ya Bungoma kufikia sasa katika kipindi cha siku tatu zilizopita.

Shule zilizoathirika kufikia sasa ni ile ya wavula ya Chesamisi na St Lukes’ Kimilili kwenye eneo bunge la Kimilili, Shule ya upili ya wavulana ya Khasoko kwenye eneo bunge la Bumula na ile ya wavulana ya Bukembe kwenye eneo bunge la Kanduyi ambayo ndiyo ya hivi punde kufuatia mgomo wa usiku wa kuamkia leo.

Kulingana na kinara wa wanafunzi katika shule ya upili ya wavulana ya Bukembe, baadhi ya sababu zilizochangia mgomo huo ni ukosefu wa dawa katika kliniki ya shule hiyo mbali na madai kuwa walimu wanawaadhibu vikali wanafunzi na hata kuwasababishia majeraha.

Aidha wameibua madai ya kupewa chakula duni huku kilio chao kutaka kusikilizwa kikikosa kufanikiwa.

Hata hivyo mmoja wa wazazi katika shule hiyo amewalaumu wazazi wenzake kwa kuwa chanzo cha utovu wa nidhamu unaoshuhudiwa shuleni, akisema wazazi hawakuwapa wanao ushauri na malezi mema wakati wa kipindi cha mapumziko.

Story By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE