Polisi huko Makueni wamemtia mbaroni mwanamme mmoja ambaye aliwaua wazazi wake kwa kuwakata kwa panga nyumbani kwao kijiji cha Muiu.
Akidhibitisha kisa hicho Jumatano asubuhi,Kamanda wa polisi Joseph Ole Napeiyan anasema kuwa wazazi wa mshukiwa walikuwa wamekatwa mara kadhaa kutumia panga.
Mshukiwa anaripotiwa kujaribu kujitia kitanzi lakini ameokolewa na kisha kupelekwa katika hospitali ya Kilungu.
Maafisa wa polisi wametembelea eneo la mkasa kabla ya kusafirisha miili katika mochari ya hospitali ya Kilingu
Mshukiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa madai mbili ya mauaji.
story by lavine Wanzetse