AFISA wa polisi, Jumanne usiku ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi waliomshambulia akiwa na mpenzi wake mtaani Land Mawe, eneo la Viwandani jijini Nairobi.

Polisi wamesema kwamba afisa huyo alikuwa na mwanamke mpenzi wake kwenye gari lake, wakati waliposhambuliwa na genge la majambazi wanne waliokuwa na bunduki wakitaka wawapatie pesa na mali nyingine ya thamani.

Inashukiwa kwamba huenda majambazi hao walilenga kumuua afisa huyo ambaye hakuwa na silaha wakati wa kisa hicho. Majambazi hao walimpiga risasi kichwani na kumuua papo hapo.

Kulingana na ripoti ya polisi, majambazi hao pia walimpiga risasi mmoja wao na kumuua walipokuwa wakipambana na afisa huyo.

Kuuawa kwa afisa huyo kunajiri huku visa vya uhalifu, vikiiwemo wizi wa mabavu vikiongezeka jijini Nairobi.

Wakati wa kisa hicho, inasemekana afisa huyo alikuwa amevalia kiraia. Polisi wanachunguza kubaini kilichofanya afisa huyo kuuawa.

Mkuu wa polisi kaunti ya Nairobi Rashid Yakub alithibitisha kisa hicho na kusema uchunguzi unaendelea

Story by Stacy Achieng

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE